SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 2 Mei 2017

T media news

Dante ‘amewachana’ wanaomsema kuhusu kujifunga

Na Zainabu Rajabu

BEKI wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ amewajibu wanaomkosoa kutokana na kujifunga kwake kwa kuwaambia kwamba hawajui soka.

Dante amejibu shutuma hizo baada ya Jumapili kujifunga bao katika mchezo wa nusu fainali ya kombe Azam Sports Federation dhidi ya Mbao na kuondoshwa kwenye mashindano baada ya kufungwa bao 1-0.

Akizungumza na Shaffihdauda.co.tz, ‘Dante’ amesema: “Mpira ni mchezo wa makosa lakini wapo watu ndani ya kikosi chetu waongea sana maneno mabaya kuhusu tukio la kujifunga lakini kwa upande wangu dhamira yangu ilikuwa kuokoa na siyo kufunga.”

“Inaniuma lakini ndiyo imeshatokea kwenye maisha utakutana na kila kitu kama vile kizuri au kibaya, kwahiyo kwangu mimi waache waongee mpaka basi ila mimi najua ni bahati mbaya,” amesema Dante.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema wamekosa kombe la shirikisho (FA) kwahiyo malengo yao kwa sasa ni kukaza kwenye ligi kuu huku akiwa na uhakika wa kushinda viporo vyao viwili vilivyobaki.