SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 15 Aprili 2017

T media news

Sanchi; Aeleza Kalio Linavyompa Mamilioni..!!!


MODO aliyejaaliwa kuwa na figa matata, Jane Ramoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa, shepu yake inampa madili ya kumuingizia mamilioni ya pesa hivyo kuweza kuyaendesha maisha yake bila presha.

Akizungumzia usumbufu anaopata kutoka kwa wanaume wakware kutokana na bambataa alilonalo, Sanchi alisema, hilo la usumbufu wa wanaume kwake wala siyo tatizo ila anachoshukuru ni kwamba figa yake inampatia pesa ndefu.

“Unajua kwa shepu hii niliyonayo, sitarajii wanaume wasini sumbue, kwa hiyo hilo kwangu wala siyo tatizo, ninachoshukuru ni kwamba napata madili ya kuwa modo kwenye video mbalimbali, matangazo na michongo mingine, kwa hiyo namshukuru Mungu kwa kunipa figa hii” alisema Sanchi.