Magoli 2 aliyoyafunga dhidi ya Bayern Munich yamemfanya Cr7 kuwa nyota wa kwanza wa soka kufunga mabao 100 katika Champions League, lakini hiyo inamfanya Ronaldo azidi kuweka rekodi mpya kila kukicha. Hizi ni kati ya rekodi nyingine alizonazo Ronaldo.
1.Hat-Trick nyingi katika La Liga. Hadi sasa Cr7 amefunga hattrick 32, hakuna mchezaji yoyote katika ligi ya Hispania La Liga ambaye ameshafunga idadi hiyo ya Hat Trick.
2.Mwanamichezo mwenye follwers wengi Twitter.Cr7 anaongoza orodha ya followers Twitter, hadi hivi sasa zaidi ya watu milioni 17 wanamfollow.
3.Mfungaji wa muda wote wa Ureno. Kama ilivyo kwa Real Madrid Cristiano Ronaldo pia katika timu ya taifa ya Ureno magoli 71 yanamfanya kuwa mfungaji bora wa timu hiyo.
4.Mfungaji wa Madrid wa muda wote. Ronaldo anaongoza orodha ya ufungaji magoli muda wote katika klabu ya Real Madrid, hadi sasa ameweka kambani mabao 324 mbele ya Raul Gonzalez aliyenga mara 323.
5.Mchezaji pekee kuwepo katika kikosi cha FIFA mara nyingi. Hadi sasa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anayeongoza kuwepo katika kikosi cha FIFA, ameingia katika kikosi hicho mara 11.
6.Mcheza soka mwenye followers wengi Instagram. Walati Lioneil Mess ana followers milioni 68 tu Instagram, Ronaldo ana followers zaidi ya milioni 95.