SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 15 Aprili 2017

T media news

Imefichuka..Malinzi na Mwesigwa Wapanga Mikakati ya Kuihujumu Simba..Waita Kamati ya Kuinyang'anya Pointi..!!!


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine ambaye sasa ni katibu mkuu wa TFF, ameitisha kikao cha kamati ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Waehezaji ambacho kinaelezwa kimepewa jina la “komboa pointi za Kagera”.

Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza, kikao hicho kimepangwa kufanyika Jumanne na kuhakikisha kinarejesha “haki” ya Kagera baada ya Kamati ya Saa 72 kuipa Simba pointi tatu na mabao matatu baada ya Kagera Sugar, kubainika ilimchezesha beki Mohammed Fakhi akiwa na pointi tatu.

“Kweli hicho kikao kimeitishwa na wajumbe wameishatumiwa email, kazi itakuwa ni moja tu kuipa Kagera pointi. Hapa nafikiri wewe hujajua ndugu yangu, Yanga wameungana na kuhakikisha iwe isiwe pointi za Kagera zinarudi. “Baba mwenye nyumba anataka pointi za timu yake zirudi, si unajua ndiye mwenyekiti wa soka Kagera.

“Wakati haya yanatokea, baba mwenye nyumba hakuwepo, alikuwa Morocco. Sasa amerudi na anataka pointi zirudi. Hapa kuna Uyanga, kumbuka viongozi wote wa juu ni Yanga. Lakini usisahau wote wanatokea hukohuko, sasa hizi pointi hata kama Fakhi alikuwa ana kadi tatu, zitarudi,” kilieleza chanzo.


EMAIL YA MWESIGWA KWENDA KWA WAJUMBE:

Kikao cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji

jm selestine <mjselestine@yahoo.co.uk>

To TPLB TPLB <tplb.tplb@yahoo.com>, Boniface Wambura <wambura70@gmail.com>

Cc Jamal Malinzi <jamalmalinzi@gmail.com>, Richard Sinamtwa <richardsinamtwa@gmail.com>

Friday, April 14, 2017 2:06 PM

Click to View Full HTML

Mtendaji Mkuu,

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).

Hii ni kukufahamisha kuwa kikao cha dharula cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF inategemewa kukaa siku ya Jumanne tarehe 18/04/2017 katika hoteli ya Protea Sea View saa 4 asubuhi.Unatakiwa kufika kwenye kikao na wafuatao:

1.Joel Balisidya

2.Rose Msamila

3.Michael Ngogo

3.Match officials wote wa mchezo wa ligi Kuu kati ya Kagera Sugar na African Lyon ie Match comm,centre ref,two assistants na mwamuzi wa nne.

4.Viongozi wa Kagera Sugar

Kila mmoja afike na nyaraka alizo nazo kuhusiana na mchezo huo.TFF itarudisha gharama za safari kwa wale wanaotokea nje ya Dar Es Salaam.

Wasalaam,

Mwesigwa Joas Selestine

General Secretary

Tanzania Football Federation