SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 11 Machi 2017

T media news

Zitambue Aina Tatu (3) Za Upendo, Dalili Zake Na Jinsi Zinavyoweza Kuathiri Maisha Yako.


Mpenzi Msomaji wa Morning Tanzania, Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere wakati wa vita vya Idd Amini, siku moja alikamata mateka, wengi wao walikuwa wanajeshi wa kutoka Libya. Basi alipowakamata alikaa nao kwa muda mrefu kidogo baadaye viongozi wa Libya walikuja wakiomba msamaha wakitaka awaachilie wanajeshi hao. Walimuuliza Mwl Nyerere, “sema tukupe pesa kiasi gani ili uwaachilie wanajeshi wetu?” Mwl alisema hivi; niambieni utu wa binadamu unaweza kuuzwa au kununuliwa kwa shilingi ngapi? Akaendelea kusema siwezi kufanya unajisi namna hiyo, kama nimeamua kuwaachilia huru nawaachilia bure kwa sababu hakuna bei ya binadamu.

Kwanini nimetoa mfano huu? Nimetoa mfano huu kwa sababu kuna mambo mawili, pesa haiwezi kuyanunua mambo hayo; jambo la kwanza utu wa binadamu na jambo la pili upendo. Hakuna thamani ya upendo wala pesa haiwezi kununua upendo hata siku moja. Kwahiyo upendo haununuliwi kwa pesa ni kitu asilia ( natural) na kina nguvu kubwa sana ya kuvunja hata miamba na hata unaweza kuponya na kuua.

Kuna aina 3 za upendo, naomba sasa tukaziangalie kwa makini na dalili zake na athari zake.

Aina ya kwanza: Upendo Wa Nafsi

Upendo huu upo kwenye kila kiumbe kilichopo duniani, kuanzia wanyama ndege wa angani, wadudu na kila aina ya kiumbe duniani. Unapomwona kuku anawalinda watoto wake ( vifaranga) ni kwa sababu anawapenda kwa upendo huu wa nafsi. Unapomwona ng’ombe anakimbia kwenda kumnyonyesha mtoto wake (ndama) ni kwa sababu ya upendo huu. Na kila kiumbe unapokiona kina mfanyia mwenzake jambo la upendo ni upendo huu unafanya kazi.

Dalili za upendo wa nafsi

-Ni upendo wa asili kila kiumbe kinao bila kujali hali yake ikoje. Kwa binadamu wakati mwingine unaitwa tamaa kulingana na mazingira unapojitokeza.

-Huibuka gafula, mtu huwaka  tamaa moyoni mwake kwa nguvu kubwa wakati mwingine hukonda au hushindwa kula au kufanya chochote punde upendo huu unapo jitokeza.

-Mara nyingi unapojitokeza kwenye swala la mapenzi, mtu hujisikia kufanya mapenzi bila woga  yaani unamfanya mtu asiogope tena kufanya mapenzi hata kama kuna hatari ya kufanya hivyo. Humwondolea mtu hofu ya Mungu dani yake.

-Haudumu muda mrefu, hutoweka haraka mfano kama umefanya mapenzi na mtu kwa nguvu ya upendo huu mara unapomaliza kufanya unamchukia mpenzi wako chuki kuu kuliko ulivyompenda.

-Watu wakiwa kwenye mahusiano hasa ya kimapenzi kwa nguvu ya upendo huu, uhusiano wao hukumbwa na migogoro mingi na mara nyingi hujawa na vivu, chuki za gafula, kukosa raha na kujuta kwingi. Kama ni ndoa haitadumu muda mrefu.

Jinsi ya kukabiliana nao unapokupeleka kubaya

Kama nilivyasema hapo juu upendo huu ni hatari sana hasa unapojitokeza kwenye swala la mahusiano ya kimapenzi. Ni vigumu kujizuia lakini unaweza kuushinda kwa mbinu zifuatazo;

-Chunga ulimi wako usitamke kitu yaani kaa kimya kwanza. Mfano unaweza leo ukamwona msichana au mvulana gafula ukawaka tamaa kali ya upendo huu jambo la kwanza ikiwa hutaki kudondoka kwenye uzinzi kaa kimya usitamke kitu. Mara baada ya muda kidogo utatoweka kabisa halafu utamwona kumbe yule mtu ulikuwa unamwakia tamaa ni wakawaida kabisa mpaka utashangaa. Kumbuka upendo huu hudumu kwa muda mfupi tu.

-Ondoka kwenye maeneo yenye uhatarishi yanayochochea upendo huu uzidi kuwaka. Ukikaa mbali na yule mtu utashangaa kwanza utasahau wala hautawaka tamaa tena.

-Usiseme ngoja nijaribishie kuongea naye. Akikukubalia kidogo tu, kwisha habari yako hamwezi kujizuia tena. Utakuja kukumbuka umeshaharibu utaanza kujuta.

-Mkioana kwa nguvu ya upendo huu, miezi kadhaa tu kwenye ndoa yenu ugomvi unaanza, ndoa yenu inaweza isidumu. Upendo huu ni kama miwani mara unapoivua miwani hiyo unabaki na macho yako ya asili utashangaa kuona kumbe mambo ni tofauti.

Aina ya pili ya upendo: Upendo Wa Mungu

Upendo huu ni wa ajabu sana, si kila mtu anaupendo huu naomba tuangalie dalili zake.

-Huanza pole pole halafu huzidi kukua mpaka unazaa matunda mema.

-Haukusukumi kutenda dhambi kamwe, hata ukijilazimsha huwezi kabisa mwili utaishiwa nguvu yaani hautaweza kabisa.

-Hudumu kwa muda mrefu, hakuna wivu, wala hasira wala chuki za kijinga ndani ya upendo huu. Ninaposema muda mrefu inaweza kuwa  miaka mingi au hata milele

-Mtu huwa yuko tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya anayempenda wala haoni hasara. Sio lazima awe mtu wa jinsia tofauti anaweza kuwa ni mama, baba, rafiki yako, au kundi la watu fulani. Ndani ya upendo huu watu huishi kwa amani na kupendana kwingi.

-Watu wakioana kwa upendo huu ndoa yao kudumu milele kwa furaha kubwa siku zote. Ndoa yao huwa paradiso

-Jinsi ya kuupata upendo huu. Huwezi ukaupata kokote isipokuwa kwa kumcha Mungu wa Mbingu na Nchi.

Aina ya tatu: Upendo Shetani

Usishangae hata shetani anaupendo wake huwapandikiza wanadamu. Anachikifanya anaiweka roho yake ya upendo ndani ya mtu na dalili zake ni hizi zifuatazo.

-Mtu huwaka tamaa kali hawezi kujizuia. Tofauti na upendo wa nafsi ambao mtu akitenda dhambi hujuta, mtu akitenda uovu kwa nguvu ya upendo huu wa shetani hajuti kamwe. Ataendelea, kama sio kila siku basi mara nyingi kutenda maovu wala hajuti kabisa.

-Upendo wa shetani unamfanya mtu ampende kila anayepita mbele yake hasa kwenye swala la mapenzi. Yeyote anayepita kwake huyo ni chakula chake hata kama awe bibi au babu. Usishangae, mara nyingi nimejionea hilo

-Kazi ya upendo huu ni kuharibu, kuvuruga, kufilisi na hatimaye kuua kabisa kwa magojwa ama kwa namna yoyote ili mradi kuua.

Jinsi ya kukabiliana na upendo wa shetani

-Sio rahisi kuushinda hivi hivi. Ukirudi kwa Mungu unaushinda, bila hivyo huwa ni ngumu sana kwa sababu kwanza upendo mwenyewe ndo huwa unakutafutia madili mazuri mazuri yanakuwa yanakujia kila siku ili usishituke. Kwahiyo kuushinda ni vigumu mpaka ukimbilie kwa Mungu hapo utaweza vinginevyo ni vigumu sana.

“Upendo mwenyewe ndo huwa unakutafutia madili mazuri mazuri yanakuwa yanakujia kila siku ili usishituke”

Tunakuhamasisha ili ufikie mafanikio yako