SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 8 Machi 2017

T media news

Za Kunyapia Nyapia... Wema Sepetu ni Mjamzito,Adaiwa Kuifanya Siri Lakini Ubuyu Wote Waanikwa Hadharani...!!!


STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ambaye alikuwapo mkoani Arusha kwa ajili ya kumsabahi Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anadaiwa kuwa mjamzito kwa sasa.

Uvumi huo umeanza baada ya kuzagaa picha za mrembo huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006 kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Picha hizo ambazo zilimwonyesha Wema akiwa na tumbo lenye ukubwa kiasi, zilizua shangwe kwa mashabiki wake wakiamini mrembo huyo huenda akawa na ujauzito.

Pamoja na maswali mengi ya mashabiki wake, Wema hakuweza kujibu chochote kuhusu madai hayo na kuwafanya wale wote wanaomuunga mkono, yaani ‘Team Wema’ kuendelea  wakizituma picha hizo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Lakini jambo kubwa lililozidi kuwachanganya mashabiki wake ni ujumbe tata wa Idrisa Sultan ambaye ni mpenzi wa zamani wa Wema ambaye aliandika: “Pigo moja tu, mbuyu chini.” Ujumbe uliozidi kuwaweka njiapanda mashabiki wa mkali huyo wa filamu.

Wema amekuwa kwenye kilio cha muda mrefu kutafuta mtoto, ambapo amewahi kubeba ujauzito wa mapacha wawili lakini haukuweza kudumu baada ya kutoka.