SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Machi 2017

T media news

Yanga Fungu la Kukosa ,Yapangwa na Waarabu Kombe la Caf...!!!


Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za kombe la shirikisho. Katika ratiba hiyo klabu ya soka ya Yanga imepangiwa kucheza na MC Alger kutoka Algeria.

Yanga imeingia katika hatua hiyo baada ya kutolewa katika kombe la klabu bingwa barani Afrika na Zanaco kutoka Zambia Jumamosi hii.

Timu 32 zimeingia katika hatua hiyo ambapo mechi zake zinatarajiwa kuchezwa kati ya April 7-9 na marudiano April 14-16. Vilabu 16 ndio vinahitajika ambavyo vitaingia katika hatua ya makundi ya kombe hilo.