Yamoto Band wiki hii wanajipanga kuachia wimbo wao mpya baada ya kumaliza tour yao ya kimataifa ambayo waliifanya katika mataifa 6.
Bendi hiyo ambayo imekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia project mpya, wiki hii itaachia kazi mpya kwa mujibu wa mkurugenzi wa bendi hiyo, Mkubwa Fella.
“Mashabiki watulie tu, muda wetu umewadia kabisa, ndani ya wiki kitu kipya tunaachia,” alisema Fella.
Alisema maandalizi ya project za bendi yako tayari na kwa sasa wanasubiri muda muafaka wa kuziachia tu.
Waimbaji hao bado kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo wao Su.