Na Zainabu Rajabu
WINGA wa Azam Ramadhani Singano “Messi” amesema goli alilofunga dhidi ya Mbabane Swallows ni zawadi kwa mama yake aliyetangulia mbele za haki.
Azam FC, wameanza vyema kampeni yao katika Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda bao moja katika uwanja wao wa nyumbani Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Baada ya mechi kumalizika, Singano aliiambia shaffihdauda.co.tz kwamba anafurahi sana pale anapocheza na kufanikiwa kufunga, kwa sababu inamuongezea kujiamini.
“Kila mchezaji ana jukumu la kufunga na kuisaidia timu pale inapozidiwa bila kujali anacheza nafasi gani uwanjani kama mimi,” amesema Singano.
Ramadhani Singano alianza kutamba na mabingwa wa zamani wa Tanzania Simba SC kabla ya kujiunga na Azam baada ya kutokea sintofaham ya kimkataba kati ya Singano na Simba.