Mbwana Samatta hakamatiki. Mchezaji huyo amezidi kuendeleza kasi yake ya ufungaji katika klabu ya KRC Genk.
Jumapili hii nahodha huyo wa Taifa Stars amefanikiwa kufunga goli moja katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata Genk wakiwa ugenini dhidi ya KVC Westerlo.
Samatta alifunga goli lake katika dakika ya saba ya mchezo huo huku magoli mengine yakifungwa na Thomas Buffel dakika ya 27, Omar Colley dakika ya 67 na Ruslan Manilovskydakika ya 90.
Mpaka sasa Samatta amefanikiwa kufunga magoli matano ndani ya wiki moja yakiwemo mawili aliyofunga Alhamisi iliyopita katika michuano ya kombe la Europa League.