SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 13 Machi 2017

T media news

Mdogo wa Lyanga anaecheza Zanaco, amewang’ata sikio Yanga

MTANZANIA anaeitumikia timu ya Zanaco FC ya Zambia Ayub Lyanga ambae pia ni mdogo wa mchezaji wa zamani wa Simba Daniel Lyanga amesema Yanga walicheza vizuri licha kupoteza nafasi nyingi za kufunga.

Zanako FC walilazimisha sare ya bao (1-1 ) dhidi Yanga kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.

Shaffidauda.co.tz ilizungumza na Ayub Lyanga na kusema kwamba, wapinzania wao siyo wabaya ila walikosa umakini katika umaliziaji wa mipira pale walipopata nafasi kwenye eneo la hatari.

“Mechi ya marudiano itakuwa ngumu, ila kwa kikosi chetu kilivyo na uchu wa kufika hatua ya makundi, hivyo basi Yanga wajipange,” alisema Ayub.

Mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga alisema hakuna mchezaji aliyekuwa anasumbua kwake ila kila aliyekuwa uwanjani amecheza kwa nafasi yake.