Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anatua nchi leo saa nne usiku.
Samatta anatua nchini akitokea Ubelgiji anakoitumikia KRC Genk ya nchini humo.
Wakati Samatta anatua nchini leo, kinda Farid Mussa ataingia nchini alfajiri alfajiri ya kesho.
Farid anakipiga katika kikosi cha Derpotivo Tenerife ya Hispania.
Wawili hao wataungana na Taifa Stars inayojiandaa kuivaa Botswana, Jumamosi kabla ya kuivaa Burundi ukiwa ni mfululizo wa mechi mbili za kirafiki.