SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Machi 2017

T media news

Maofisa mawasiliamo wa serikali watakiwa kuhuisha tovuti za umma

Serikali imewaagiza maofisa mawasiliano na wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa umma kuhakikisha kuwa tovuti za umma zinahuishwa kwa wakati ili kuzuia watu kueneza na kufanyia kazi  taarifa zisizo sahihi.

Akizungumza leo mjini Dodoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge alisema  kama watu  hawajapata taarifa sahihi na kwa wakati watalazimika kufanyia kazi taarifa zisizosahihi.

“Hali si nzuri katika baadhi ya tovuti utakuta zimehuishwa mwaka jana kwa mara ya mwisho. Mtu akitaka taarifa ni lazima apige simu sasa mfanye mabadiliko kwa kuhakikisha kuwa taarifa zinakuwa katika tovuti kwa wakati,”alisema.

Alisema katika kuhakikisha kuwa maofisa hao wanakuwa na uelewa, Serikali kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimarekani (USAID) wamewapa mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa mawasiliano na Tehama wa umma.