SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 12 Machi 2017

T media news

Mambo Yaliyopelekea CCM Kuwatimua Makada Wake 12 Yafichuka..!!!!


Kuna mambo kadhaa yanayoweza kuhusishwa na uamuzi mgumu ilioufanya CCM wa kuwafukuza wananchama wake 12 uliofikiwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho mjini Dodoma.

Katika uamuzi huo, chama hicho kimewatimua wanachama hao wakiwa ni viongozi wa juu ambao walikuwa na nyadhifa za juu za kiuongozi, wakiwamo wenyeviti wa mikoa na wilaya.

Hata hivyo, uamuzi huo unaweza kuwa na msukumo wa CCM kupoteza majimbo mengi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, huku kura za urais pia zikipungua tofauti na zile alizopata mgombea wake mwaka 2010.

Kabla ya mkutano huo ulinzi ulitawala katika eneo la ukumbi wa mikutano ukihusisha walinzi wa chama hicho na pia maofisa usalama kutokana na unyeti wake.

Vilevile, kabla ya mkutano wa NEC, Mwenyekiti wa chama, Rais John Magufuli aliingia ukumbini akiwatangulia wajumbe wote kwa dakika 14.