SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 9 Machi 2017

T media news

Makonda aenda mapumziko ya miezi miwili Afrika Kusini

Wakati utata ikigubika safari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda nchini Africa Kusini, imebainika kuwa kiongozi huyo atakuwa likizo nchini humo kwa zaidi ya miezi miwili.

Kwa mujibu wa habari ya gazeti la TanzaniaDaima imeeleza uwepo wa RC Makonda nchini Afrika Kusini ndio sababu ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya maandismisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo ilitangazwa kuwa angekuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizofanyikia uwanja wa Mwembeyanga.

Kuondoka kwake nchini kumekuwa kwa kutatanisha wakati mamlaka husika zikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusuana na safari yake. Wadadisi wa mambo wanahoji uhalali wa Makonda kupewa mapumziko hayo nje ya nchi huku serikali ilitangaza kuzuia zara zote za watumishi nje ya nchi ili kubana matumizi.

Kutokana na zuio la safari za nje ya nchi kwa watumishi wa umma lililotolewa na serikali ya awamu ya tano, safari hiyo ya Paul Makonda imeibua utata juu ya uhalali wake huku mamlaka husika zikikwepa kuzungumzia safari hiyo.

Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas alipoulizwa kama safari ya Makonda nje ya nchi yupo kikazi au binafsi alisema kuwa swali hilo aulizwe, Katibu Tawala wa Mkoa kwani ndiye mtendaji wake. Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando alipoulizwa alisema kuwa, swali hilo atafutwe Makonda mwenyewe.