SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 7 Machi 2017

T media news

Leo, Tarehe 7/3/2017 M/kiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dr. Antony Diallo amefanya ziara ya kichama katika Wilaya ya Ukerewe_



M/kiti *Dr. Diallo* amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ukerewe kwa kukutana na madiwani wote wanaotokana na chama cha mapinduzi.
Lengo la ziara hiyo ni kubaini changomto zinazowakuta madiwani pindi wanapotekeleza ilani ya chama cha mapinduzi , lakini pia kuangalia na kutathimi utekelezaji wa ilani ya CCM katika maeneo yao.

M/kiti wa CCM aliwataka viongozi wa CCM kuendelea kuhakikisha wanawasimamia vyema madiwani hao ili waweze kutekeleza ilani ya ccm.


Pia m/kiti ameitaka Halmashauri zote kupitia Wilaya ya Ukerewe watenge asilimia kumi 10% za mapato yanayopatikana katika halmashauri zao kwaajili ya vijana na wakinamama ili wajikwamue kiuchumi.
M/kiti aliongezea kwa kusema kuwa hiyo asilimia tano ikitumika vizuri kwa vijana siamini kwamba bado vijana wataendelea kupiga kelele kuhusiana na swala la ajira maana wataweza kujiajiri vizuri.

Pia m/kiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe comrede *Ally Mambile* alimshukuru saana m/kiti wa CCM mkoa wa Mwanza kwanamna anavyokuwa akiwatembelea mara kwa mara katika Wilaya hiyo.
Na kumhakikisha sipidi hii ikiendelea anaimani 2020 jimbo la Ukerewe litarudi ccm.

Mwisho.
M/kiti wa ccm mkoa wa Mwanza *Dr. A. Diallo*aliwataka viongozi wote kufanyia kazi maelekezo aliyoyatoa na kuitaji Taarifa za uhakika dhidi ya maelekezo hayo.

*Imetolewa na*
*Ofisi ya ccm*
*Wilaya ya ukerewe*
*Mwanza*