SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 8 Machi 2017

T media news

Jokate Mwegelo Aanzisha Mafunzo Ya Ujasiriamali Kwa Wanafunzi Wa Kike

Mrembo mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango maalum wa kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Jokate ataanza mafunzo hayo maalum kwa wanafunzi wa kike kuanzia wiki ijayo na lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ufahamu wanafunzi hao na kuanzisha biashara zao mara baada ya kumaliza elimu yao ya sekondari.

Alisema kuwa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi ni muhimu kwani yanawawezesha kujiandaa vizuri kukabiliana na maisha mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya ngazi ya juu.Kwa mujibu wa Jokate, unaweza kusoma mpaka Chuo Kikuu ndani na nje ya nchi, lakini bado utakabiliana na ugumu wa kupata ajira ambazo kwa sasa ni haba.

“Kuna wengine wamesomea taaluma fulani  kwa ngazi ya Chuo Kikuu lakini mpaka sasa hawana ajira na kukata tama katika maisha, pia unaweza kufanya kazi tofauti na taaluma uliyosomea, lakini kwa ujasiriamali ni tofauti, utajifunzi jinsi ya kupata mtaji, kukopa na kurejesha, kufanya biashara gani na mbinu zake,”

Jokate Mwegelo akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai ya Ilala wakati wa mahafari ya mwaka .