Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Mwana Hip Hop Afande Sele TheKing ametoa ya moyoni baada ya Kuibuka Tetesi za Uvamizi wa Clouds Media.Kupitia Ukurasa wake wa Facebook Msanii huyo ambaye ndie mfalme wa kwanza wa Miondoko ya Kufokafoka nchini ameandika ya fuatayo:-
“Kama ni kweli Bashite ameongoza watu kufanya uvamizi kwenye kituo cha clouds media kwa jinsi inavyojieleza…Basi atakua mfano wa tumbili aliyemaliza kurukia miti yote sasa ameamua kurukia mwili wa anaemfuga…Na’Anko’akiendelea kushupaza shingo ktk hili huenda yale maandiko yakatimia kabla ya muda tarajiwa…muwe na Jpili Kareem akina ndugu…..” – Afande sele aliandika kupitia akaunti yake ya Facebook.
Hii hapa Original Post.