Zitto atinga mahakama ya Kisutu kumsapoti Lissu.
Leo Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrisa na Simon Mkina wanaendelea na kesi inayowakabili.
Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washitakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Katika shtaka la pili alidai washatakiwa , Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Shtaka la tatu linamkabili mshtakiwa wa tatu, Mehboob ambaye anadaiwa kuwa Januari 13 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.
Alidai mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.