Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano, jijini Dar es Salaam.Shear Illusion kupitia bidhaa yake ya manjano imeanzisha mpango maalum wa kusaidia kutoa ajira kwa wanawake ambao wamemaliza shule na kushindwa kupata kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Manjano na Kampuni ya Shear Illusions Ltd, Shekha Nasser amesema ameamua kumualika Waziri Mwijage ili aweze kuona fursa zilizopo katika viwanda vidogo vidogo
Amesema kuwa mara baada ya kuona tatizo hilo wakaamua kuanzisha mradi wa uuzaji wa bidhaa za manjano kwa wanawake mbalimbali waliopo jijini Dar ese Salaam na mikoa mingine.
“tasnia hii ya urembo ni moja ya vitu vinavyoweza kumsaidia mwanamke kuingiza zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi kama mtu atakuwa mwaminifu na biashara na kuifanya hii kuwa ni kazi yake ya muhimu katika kujikwamua kiuchumi” amesema. Shekha Nasser
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Manjano na Shear Illusion LTD, Shekha Nasser akizungumza na waandishi wa habari wakati kutangaza uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano, Jijini Dar es salaam leo.Amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wasichana hao wameamua kutoamafunzo ya wiki mbili kwa wasichana 30 ambao watapewa mtaji wa shilingi 300,000/-Amesema kuwa wasichana hao ambao wapo 30 wamepatikana kutokana na mchujo uliofanywa na watalaamu wa masuala ya urembo hadi kufikia hapo.
Sehemu ya Washiriki waliofuzu kujiunga na mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano.