SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Februari 2017

T media news

WAKILI WA WEMA AFUNGUKA HAYA JUU YA WEMA SEPETU

Mwanasheria wa Wema Sepetu, Albert Msando amefunguka na kusema kuwa kuna watu ambao hawajapendezwa kuona ameingia katika kesi ya Wema Sepetu na kwenda kumsaidia kisheria.
Albert Msando anasema wale wote ambao wameungana na kupigana naye vita kisa tu amekwenda kumsaidia Wema Sepetu wanapaswa kutambua kuwa Wema Sepetu ni kama mtu mwingine ambaye si mkamilifu ila si mtu mbaya na ana moyo wa upendo.

Albert Msando & Wema Sepetu
“Ushawahi kuwa na dada ambaye yupo tofauti na wewe? Rafiki ambaye huwezi hata kuelezea kwanini ni rafiki yako? mimi ninaye ambaye ni Wema Sepetu, Kuna watu wameongea walichoongea. Wamekasirika mimi kumsaidia Wema. Ila ukweli unabaki kwamba Wema Sepetu has her following. lazima nimesem yeye kama ilivyo mimi na wewe sio mkamilifu. She has her share of mistakes. And failures. But she is not a bad person. She has a special heart.” aliandika Albert Msando. 

Mbali na hilo Msando amesema kuwa kitu anachokifanya yeye ni kumsaidia na kumuongoza Wema Sepetu kuwa mtu mzuri licha ya makosa yake na kutambua uwezo na thamani yake na kufanya jambo hilo siyo sheria tena bali ni urafiki.
“Kwa hiyo kwa wale ambao wameamua kupigana vita kwa kuniattack I am leaving it to them. For me all I have to do is, guide her to being better and realising her full potential. Thats not law. Thats friendship” aliandika Albert Msando.