SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 23 Februari 2017

T media news

VAZI LA BEYONCE NI NDOTO ZA VIJANA KUMI WANOWAZA KUMILIKI GARI BONGO.

Inawezekana kabisa usiwe mfuatiliaji wa michezo kabisa lakini unapenda mitindo na Urembo sana. Katika mchezo wa Kikapu uliojumuisha Wachezaji mashuhuri kutoka West na East katika NBA AllStars ni mchezo uliovuta watazamaji wengi sana akiwemo Jay Z na Mkewe Beyonce na hapa nyumbani alikuwepo mwanamitindo Jokate Mwegelo. Achana na wahudhuriaji wa mechi ile, leo tunaakisi mavazi aliyotupia Mama kijacho tena wa watoto mapacha Mrs Carter Beyonce alivalia vazi la gharama sana asili ya Japan lenye thamani ya zaidi ya dola elfu 22,000 sawa na shilingi milioni 48 za kitanzania vazi hilo la Kimono lililohaririwa kwa silki pamoja na manyoya ya chui lilibuniwa na kampuni ya Gucci, kibongo bongo Vazi hili linaweza kuwafanya washikaji kama kumi na moja kila mtu akamiliki gari aina ya IST na akasumbua mjini hapa. Tizama hapa kwa ukaribu Vazi Lenyewe.