SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 13 Februari 2017

T media news

RAY C ASEMA HAYA JUU YA RECHO KUTAJWA KWENYE ORODHA YA MH PAUL MAKONDA

Ikiwa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajia kutaja majina mengine ya vinara wanaotuhumiwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.

Msanii Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye ametamba kwenye anga la Bongo Fleva kwa siku nyingi, amefunguka na kutoa ya maoni baada msanii Recho ambaye amekuwa akifuata nyayo zake kuhusu kutajwa kwake kwenye orodha ya watu wanaohusika na dawa za kulevya.

Ray C

Kupitia FNL, Ray C alidai hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana uhakika juu ya suala hilo.

“Mimi Recho namjua vizuri, lakini kutokana na matatizo yangu sijaonana naye muda mrefu sana, sipo hapa kumzunguzia mtu, na siyo vizuri, pia siyo vizuri kuzungumzia kitu ambacho sina uhakika nacho maana mimi sijawahi kumuona akitumia hiyo kitu.

Aliongeza, “Nachoweza kusema ni kuwa kama mimi niliweza, kila mtu anaweza, naamini atakuwa poa maana najua ni mwanamke imara”.