SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 13 Februari 2017

T media news

HAYATOU APATA MPINZANI CAF


CECAFA, imemmteua Ahmad Ahmad kuwa mgombea wa nafasi ya Urais katika Shirikisho la mchezo wa soka barani Africa (CAF) katika uchaguzi unaotaraji kufanyika mwezi march.

Uamuzi wa CECAFA kumuunga mkono Ahmad natokana na maadhimio yaliyoafikiwa katika mkutano wa siku ya uliofanyika siku ya Jumamosi huko Johannesburg.

Ahmad, ambae ni Raisi chama cha soka nchini Madagascar tayari ameshaweka wazi ya kuwania kurithi mikoba ya Rais wa sasa wa Issa Hayatou katika uchaguzi utakaofanyika Ethiopia.

Issa Hayatou, amekuwa akiliongoza shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF tangu mwaka 1988 na sasa anataka kutetea nafasi yake ili aliongoze shirikisho hilo kwa muhula wa nane.

Mwaka uliopita Caf ilipitia sharia mpya ya ukomo wa madaraka kuwa misimu mitatu ya miaka mine kwa kila msimu, hivyo Hayatou anaweza akaiongoza tena Caf kwa miaka 12 zaidi.