MKuu wa Mkoa AELEKEZA safari za kikazi kwa watumishi wa serikali Mkoa wa Mbeya kutumia shirika la Ndege la Taifa(ATCL)
- Asema Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe Ukikamilika utakuwa ni lango la kuingia Tanzania kwa nchi zote za kusini mwa Afrika
- Ameiomba ATCL watakapoingiza Ndege nyingine kuweka katika Mipango YA safari za Mbeya - Malawi- Dar
Uongozi wa shirika la Ndege la Taifa( Air Tanzania) umehaidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini kote ikiwa ni sehemu YA mikakati yake YA kibiashara
Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti wa bodi YA ATCL Ndg Emanuel Koroso na Mtendaji Mkuu wa ATCL Eng Ladislaus Matindi walipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla
Wamewashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Mbeya na watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano wanawapa wa kutumia shirika hilo ktk Safari zao na wamewaomba kuendelea kulitumia shirika hilo ambalo limeboresha huduma zake
Mkuu wa Mkoa amelishukuru shirika la Ndege kwa kuweka Mkoa wa Mbeya ktk Safari zake na kufanya hivyo limepunguza kero YA wananchi kukwama kusafiri kama ilivyokuwa hapo awali
Aidha ameliomba shirika hilo kuweka ktk Mipango yake watakapopata Ndege zingine kutoa huduma kwa nchi za jirani ikiwemo Malawi na zambia kwa kupitia uwanja wa Ndege wa songwe