Aingilia kati mradi ulikwama kwa miaka 8
- Asema mradi umekuwa ukisuasua kwasababu Nyingi ikiwemo mapungufu YA usanifu, migogoro YA kisheria na wakandarasi na uzembe wa usimamizi
- AHAIDI kuwachukulia hatua wote watakaoukwamisha mradi huo
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewahaidi wananchi wa Vijiji 15 kuwa serikali YA Mkoa imeamua kufuatilia na kusimamia kwa Karibu mradi wa Maji masoko utekelezwe na wananchi wapatao 62,000 wa Vijiji 15 katika kata 5 wanufaike na Huduma YA Maji
Aidha amewaomba radhi wananchi kwa kuchelewa kukamilika kwa mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 4
Amesema mradi huo umekuwa ukisuasua kutokana na mapungufu YA kitaalamu, migogoro YA kisheria na wakandarasi na uzembe ktk usimamizi
Amehaidi kuwa ofisi yake imeamua kufuatilia kwa Karibu mradi huo mpaka ukamilike na amewataka watumishi idara YA Maji kuongeza umakini katika usimamizi na yeyote atakayezembea au kuhujumu mradi huo atamchukulia hatua