SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

T media news

UTOAJI WA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA (LEGAL AID) KWA WANANCHI WA MKOA WA DARA ES SALAAM



Wakati wa wa ziara yangu ya siku 10 niliyoifanya ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 19/11/2016 hadi tarehe 28/11/2016 kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi niligundua mojawapo ya changamoto zinazowakabili wananchi wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam ni;-

(i) Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu sheria kiasi cha kupelekea kupoteza haki zao za Msingi kisheria.


(ii) Malalamiko ya rushwa katika vyombo vinavyojihusisha na utoaji wa haki

(iv) Waajiri kuwaachisha/kuwafukuza kazi Waajiriwa katika sekta binafsi bila kufuata sheria,kanuni na taratibu.

(iii) Ucheleweshaji wa kesi Mahakamani

(v) Migogoro ya Ardhi

(vii) Mirathi nk.

(vi) Migogoro ya Ndoa

Changamoto hizo zimetokana au zimechangiwa kwa sababu ya wananchi wengi kukosa msaada wa kisheria. Kukosekana kwa msaada wa kisheria unaweza kumfanya mtu kuhukumiwa au kupoteza haki yake ya kimsingi kisheria.

Licha ya uwepo wa wadau wa kisheria/vituo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambavyo vinafanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam wananchi wengi wameshindwa kufikiwa kwa wakati kiasi cha kusababisha wananchi wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhangaika zaidi kwa kutafuta huduma ya Msaada wa Kisheria .

Kutokana na umuhimu wa huduma hiyo niliona ni vema wakapatikana vijana (35) ambao wana utaalamu wa kisheria katika Mkoa wa Dar es salaam ili waweze kuwasaidia wananchi wa Dar es salaam ambao wengi wanapoteza haki zao kwa kwa kutokujua sheria,jambo ambalo linatimiza azma ya Serikali ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria na kupata haki bila ubaguzi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kuhusu haki zao.

Vijana hawa wataalam wa sheria tulionao hapa ni zao la mchakato wa muda mrefu uliohusisha kuangalia uwezo wao wa ufaulu katika maswala ya sheria,utayari wa kutoa huduma na hali nzuri ya kuhudumia wateja (customer care).

Tumetumia njia ya kuwachuja kiuwezo ili tupate wataalam wazuri na kamili. Pia tumewapa vijana hawa mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma kupitia wataalam wetu hapa mkoani.

Wajibu wa vijana hawa ni kufanya haya yafuatayo÷

Uwepo wao kama vijana waliojitolea kufanya kazi hii katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam itarahisisha huduma hii kwa wananchi ambao hawafikiwi na huduma ya kisheria wanapohitaji ikiwa ni kauli mbiu “popote uwepo utafikiwa”.

Hivyo basi, kutokana na imani ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoonyesha mbele yao kwa kuwachagua ili waweze kwenda kuwasaidia wananchi kwa kuwapa msaada wa kisheria.(Legal Aid)

(ii) Wananchi watakuwa wanashiriki moja kwa moja katika kupunguza mlundikano wa mashauri yaliyopo Mahakamani.

(i) Kutoa huduma za kisheria kwa wananchi kwa Wilaya zote (ii) Kutoa msaada wa kisheria (Legal Aid) kwa watu na makundi ya watu wasio na uwezo katika mashuari ya madai ya jinai.

(iii) Kushughulikia malalamiko mbalimbali juu ya utoaji haki kutoka kwa wananchi

(iv) Kuwaelekeza pamoja na kuwaelimisha wapi waende kupata suluhu ya haki zao

(v) Kuwandika nyaraka tofuati za kisheria zinazohitajika kukamilisha mchakato wa kisheria kama kuandika WOSIA mikataba nk ikiwa na kutoa msaada wa kisheria kwa njia ya simu.

Serikali inategemea nini kutoka kwa vijana hawa÷ (i) Serikali inataka wananchi wawatumie katika kutatua migogoro yao mbalimbali ya kisheria wanayokabiliana nayo ili kuepuka kupeleka Mahakamani migogoro ambayo inaweza kusuluhishwa nje ya Mahakama.

DAR ES SALAAM

(iii) Uwepo wao utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa ukaribu katika maeneo yao na kupata msaada wa kisheria katika maeneo waliyopo kwa manufaa ya wananchi

ASANTENI SANA. PAUL C. MAKONDA

MKUU WA MKOA