SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

T media news

LICHOKISEMA MAMISA BAADA YA YOUNG DEE KUMKUBALI MWANAYE


Kuanzia Ijumaa iliyopita ishu iliyokuwa ikitrend zaidi kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu rapper Young Dee kumkataa mtoto ambaye amezaa na msichana afahamikae kama Mamisa.

Picha liliendelea baada ya Young Dee kumkubali mtoto huyo na kuahidi kutoa huduma zote kama Baba. Haikuishia hapo tu, mapicha picha kuhusu wasichana ambao wamewahi kusikika kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Young Dee (Tunda na Amber Lulu) kufananishwa na mzazi mwenzake huyo na Young Deendio kitu ambacho kili trend kinoma noma wiki hii nzima.

Hadi kupelekea mrembo Tunda kutoa POVU lisilo la polepole katika page yake ya Instagram na kulaani vikali kitendo cha yeye kufananishwa na wasichana hao wenzie.

UNAJUA KUNA WAKATI MWINGINE IFIKE WAKATI KUJUANA HUMU INSTA ISIWE TABU!..NAONA IMEFIKIA HATUA YA KUFANANISHANA NA VITU VYA AJABU SASA JAMBO AMBALO HALIMPENDEZI HATA MUNGU HIVO NAOMBA KUTOA ONYO SITAKI KUSHINDANISHWA N VITU VYA AJABU HALAFU KWA MAMBO YA KIJINGA YASIONIHUSU!..MSINILAZIMISHE KUMKOSEA MUNGU

A PHOTO POSTED BY BOSSBABE
/APPLE (@OFFICIAL_TUNDA) ON DEC 13, 2016 AT 9:59AM PST


Hakuwahi kusikika popote mrembo Mamisa kuzungumzia suala hilo, lakini leo U-Heard ya XXL imempata exclusive na kafunguka mengi sana baada ya Young Dee kumkubali mtoto wake.

Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mahaba moto moto baina ya wawili hao yamerejea kama kawa na Young Dee yupo katika mipango ya kumchukua kabisa bibie Mamisa na kuishi naye ili wamlee mtoto wao.