SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

T media news

AKAUNTI YA MTOTO WA STAA DIAMOND PLATNUMZ YAFIKISHA MA FOLLOWER 56,756

Mtoto wa pili wa Diamond Platnumz, Prince Nillan ameendelea kuwa maarufu katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kufikisha followers 56,756 ikiwa ni siku 10 toka mtoto huyo atambulishwe kwenye mtandao huo.

Mtoto huyo alizaliwa saa 10 na dk 35 Alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki, Jumanne, December 6.

Diamond amekuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaendesha maisha yao kibiashara.

Diamond akiwa na mtoto wake, Prince Nillan

Mtoto wa kwanza wa muimbaji huo, Princess Tiffah ambaye ana followers milioni 1 katika mtandao huo, alianza kupata deal kubwa za matangazo katika umri mdogo.

Kwa sasa watoto hao bado wanaishi na mama yao Zarithebosslady nchini Afrika Kusini.