SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

T media news

JOHN LEGEND: KANYE WEST KUKUTANA NA DONALD TRUMP ILIKUWA NI KIKI TU

Wiki hii stori kubwa ilikuwa ni kukutana kwa Kanye West na Rais mteule wa Marekani Bw.Donald Trumpkwa mara ya kwanza tangia autangazie umma kuwa angepiga kura angempigia Trump.

Leo jarida la Lovebscott la Marekani limefanya Exclusive Interview na Rafiki yake wa karibu kutoka G.O.O.D MUSIC John Legend.

Moja ya vitu walivyo zungumza ni kuhusu ishu ya Kanye West kukutana na Donald Trump, yeye amesema kaichukulia kama Kiki kwani anamjua vizuri Kanye West yuko tofauti na watu wanavyodhani.

“Siko hapa kuzungumzia ishu za Trump, ila nafikiri Kanye west kukutana na Donald Trump ilikuwa ni KIKI tu hakuna lolote la ajabu, mimi namfahamu Kanye ingawaje ni kweli aliwakatisha tamaa mashabiki wake baada ya kutamka angempigia kura lakini hiyo haibadilishi maana tuache kama yalivyo tu” Alisema John Legend .