SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 2 Desemba 2016

T media news

Baraza la wadhamini lamtaka Makonda kusimamisha mkutano wa dharura Simba

Dar es Salaam. Baraza la wadhamini la klabu ya Simba limemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuingilia kati na kuusimamisha mkutano mkuu wa dharura mpaka uongozi utakapokutana na baraza hilo.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Hamis Kilomoni amesema baraza hilo limefikia hatua hiyo baada ya kupokea barua za  malalamiko kutoka kwa wanachama.

"Kama wadhamini tumepokea barua za wanachama wakilalamikia kutoitwa katika mkutano uliopita. Barua hizo zimepelekwa kwa rais,BMT hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa aingilie katika na kusimamisha mkutabo mpaka viongozi wakutane nasi,"amesema

Kilomoni amesema baraza la wadhamini halitambua mkutano huo na kwamba ni batili.