SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

T media news

BAADA YA KUTUA AIRPORT DSM, BEN POL KAELEZA SHOW YAKE YA UJERUMANI ILIVYOACHA HISTORIA.



Usiku wa December 14 2016 msanii wa Bongofleva Ben Pol aliwasili Dar es Salaam Tanzania akitokea Frankfurt Ujerumani, alipokuwa ameenda kufanya show katika mji wa Offenbach UjerumaniBen Pol amerejea Dar es Salaam na kuelezea mapokezi ya muziki wake Ujerumani.

Show yake ya Offenbach Ujerumani ndio show yake bora katika maisha yake hiyo inatokana na kufanya show hiyo akiwa msanii pekee yake na live band ya hapo, show hiyo Ben Pol ameeleza kuwa haikuwa na waafrika ilikuwa na wajerumani na walionesha kukubali zaidi hit single yake ya ‘Moyo Mashine’

Ben Pol ameeleza kuwa show ya Offenbach ilihudhuriwa na watu wanaofikia 10000 na imeacha historia katika maisha, huku kukiwa na watanzania watatu pekee, yeye mwenyewe, Emmanuel Austin na mjomba wa Emanuel Austin.