WAZIRI WA HABARI NCHI KONGO DRC LAMBERT MENDE
SHERIA mpya nchi DRC Kongo yavitaka vyombo vya habari visivyo vya nchi hiyo kuacha kufanya kazi. sheria hiyo itaanza kufanya kazi mwisho wa wiki hii ambapo vyombo vya habari vya BBC na RFI vitaathirika moja kwa moja na sheria.
hata Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wao kufuatia sheria mpya nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambayo inavitaka vituo vya habari vya kigeni kujiandikisha kama makampuni ya nchi hiyo la sivyo matangazo yao yazimwe
Sheria hizo mpya zitaanza kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.
Vyombo vya habari vya kigeni sasa vitaruhusiwa kutangaza nchini DRC, ikiwa asilimia kubwa ya wenye hisa ni raia wa Congo.
Maafisa wamevipa vyombo hivyo muda wa siku 30 kutekeleza matakwa hayo
Sheria hizo zinaathiri vituo kama Radio France Kimataifa (RFI) Sauti ya Amerika na BBC.
Matangazo ya RFI kwa sasa yamezimwa nchinin DRC, tangu itangaze mipango ya upinzani ya kufanya maandamano mapema mwezi ujao