SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 18 Novemba 2016

T media news

UKWELI KUHUSU PAPA KURUHUSU TALAKA KWA NDOA ZA KANISA KATOLIKI

Wenzetu nchi zilizoendelea waandishi wa habari wanaoandika habari za aina fulani ni lazima wawe ma uweledi wa jambo hilo.Ukiwa unaandika habari za uchumi,basi ni lazima walau uwe na ABC za mambo ya uchumi,siasa kadhalika,habari za afya na hata zile za mambo ya uhandisi.Ndio maana si ajabu kukuta mwandishi wa habari kaandika habari za mambo ya usafiri wa anga,akaandika "Kutana na mwanamke wa kwanza kurusha ndege aina ya BOEING AIRBUS".Wakati kiukweli hakuna aina ya ndege hiyo duniani.

Habari za kanisa,pia zinahitaji walau mwandishi awe na ABC za mambo ya kanisa na kupata ufafanuzi wa uelewa wa mambo mengi ndani ya kanisa.

Kuna habari inazagaa,na imetolewa ufafanuzi makanisani,sio kweli kuwa Papa ameruhusu "Talaka" kwa ndoa za kanisa katoliki,ila ukweli ni kuwa Papa amerahisisha njia za "utatuzi wa migogoro" ya ndoa ndani ya Kanisa Katoliki.

Ifahamike kuwa toka miaka na miaka,ndoa za kanisa katoliki zimekuwa zinafuata mlolongo mrefu pale zinapoonekana kuwa zina hitilafu ili kuweza kuwa "invalid".Kutokana na elimu ndogo juu ya sheria za ndoa ndani ya kanisa kwa waumini,wapo waumini wengi wanaodhani hawawezi kubatilisha ndoa zao hasa kama zilifungwa bila kufuata vigezo.

Sasa badala ya maamuzi haya kufanyika Vatican kwenye Mahakama ya Ndoa "Rota Romana" sasa jambo hili limaweza kuwa mikononi mwa Askofu Mkazi.Hivyo kuondoa ule mlolongo wa mtu kutoka kigango cha Luhumbo Kishapu Jimbo la Shinyanga kwenda Rota Romana Vatican na sasa mtu huyo ataenda Cathedral Ngokolo Shinyanga kupeleka shauri lake.Huu ndio msingi wa ujumbe wa Papa,kuleta madaraka katika majimbo mahalia.

Kuna kutazamwa kwa ndoa zilizobatilishwa kwa namna mbili,ya kwanza ni "Annulamento",hii ni ndoa inayotenguliwa mahakama za kiraia lkn kanisa linakuwa kinaendelea kuitambua kama ni ndoa "valid" sbb kuharamishwa kwake hakujafuata taratibu na sheria za kanisa,bali za kidunia.Mahakama huzibatilisha ndoa hizi kutokana na "magumu ya dunia".Hivyo Mahakama za kidunia hutalakisha ndoa ambayo ni "valid" kikanisa.Kanisa katoliki inawachukulia watu hawa ni wanandoa,na hiyo inakuwa ni "impediment" kwa wao kufunga ndoa nyingine.

Namna ya pili ni "Nullità",kingereza ni "Nullity".Nullity maanake hiyo ndoa toka "inazaliwa" haikuwa ndoa halali na hivyo kanisa inaibatilisha.Ndiyo maana kanisa katoliki hutangaza ndoa husema "wenye kizuizi",na matangazo huwa kwa muda mrefu na hutangazwa mahali pote wanandoa walipowahi kuishi.

Kuna sababu za Mahakama ya Kanisa ku-nullify ndoa iliyofungwa kanisani,sababu hizo ni kama vile

Uhuru,iwapo itathibitika pasi na shaka kuwa mmoja kati ya wanandoa alilazimishwa.Kumficha mwenzako kama ulikuwa na watoto njeKuficha kuwa upo huru wakati ulishafunga ndoaKuwa impotent (hanisi/tasa) bila uwazi kablaKwa Padre kufunga ndoa na mwanamke bila yeye kusema ni padre

Ili mtu upate kibali cha kufunga ndoa ya pili hizo juu ni sababu mojawapo katika kanisa katoliki, inabidi upate kibali kutoka katika "Mahakama ya Kanisa".Hizi mahakama za "Nullity of Matrimony" zipo katika kila Jimbo Tz,huundwa na mahakimu watatu ambapo hata walei wanaweza kuwepo lkn katika hao watatu ni mkleri ambaye anatakiwa awe kiongozi.

Askofu wa Jimbo lolote anaweza kutoa "nullity" kwa ndoa zile ambazo evidence zake zipo wazi.Kila jimbo palipo na askofu tayari ile ni mahakama.Sasa Maaskofu wanaweza kukubaliana wakaunda mahakama moja inayojumuuisha majimbo kadhaa.Mfano Mahenge,Kilosa na Morogoro wakawa na mahakama moja.

Na katika kila shauri la "Nullity of Matrimony" huwa yupo Padre mwingine kwa ajili ya "defend of matrimony",ambaye lazima awe padre aliyebobea katika sheria za kanisa(Canon law).Na hata wakitokea wanandoa wanakubaliana yeye huwa against na huweza ku-appeal mahakama ya juu ili ndoa hiyo isiweweze kuwa "invalid"

Kuna muundo wa Kimahamaka pia ndani ya kanisa,toka Mahakama ya mwanzo hadi rufaa.Hii huanzia kwa mahakama za kijimbo,ikishindikana shauri hupelekwa kwenye mahakama ya Metropatania(Jimbo Kuu),hapo ikishindikana shauri hupelekwa kwa Askofu Mkongwe(Kwa umri) ktk eneo husika na rufaa ya mwisho huwa Rota Romana Vatican.

Wenzetu wa nchi zilizoendelea,ambao elimu ya sheria za kanisa hutolewa kwa waumini wa kawaida kwa nafasi na uwazi,mambo haya wanayafuatilia na kufahamu.Wapo wakristo Afrika ambao ndoa zao ni "invalid",lkn kwa "kukaririshwa" kuwa ndoa za Kanisa ni mpaka "kufa na kuzikana" basi wanaendelea kukaa katikati ya uvuli wa mauti,lkn kumbe wanaweza kufuata hatua hizi na endapo ikathibitika pasi na shaka,basi ndoa zao zinakuwa "Nullified".Sasa Papa kapunguza mlolongo huu,na sio karuhusu "talaka"

Zamani mashauri haya yote yaliruka moja kwa moja mpaka Rota Romana,Vatican,lkn sasa imerahisishwa,kurahisishwa huku kwa kuanzia ngazi ya Maaskofu,basi waandishi wasiotafiti wanaishia kusema "Papa aruhusu Talaka ndoa za kanisa Katoliki".