Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).
Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki.
TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.
Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama ifuatavyo:
Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali. Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.
Mwisho, Mamlaka inawasihi wananchi kuepuka kutumia Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe:huduma@tra.go.tz
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu