Klabu ya Simba SC imesema imeanza kuwangozea mikataba baadhi ya wachezaji wao akiwepo Mohamed Hussein maarufu kama Tshabalala. Afisa habari wa klabu hiyo alithibisha taarifa hiyo wakati akizunguza na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Taarifa ya Tshabalala na Mkude pamoja na wachezaji wote ambao wako Simba taarifa zao zipo ndani ya klabu na wataendelea kucheza Simba. Mchezaji ambaye bado anahitajika na klabu na yupo kwenye mipango ya kocha na uongozi ukaafiki, ataendelea kucheza ndani ya Simba kwahiyo hao wote bado tunamipango nao,” Manara amewatoa hofu wanachama na wapenzi wa Simba baada ya tetesi huenda baadhi ya wachezaji wakaikacha klabu hiyo.
“Deal ya Tshabalala tayari imeshafungwa, anaendelea kucheza kwenye klabu ya Simba. Taarifa rasmi kuhusu usajili wa Simba, tutazungumza Jumatatu.”
Awali kuna habari zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda mlinzi wa kushoto wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ atajiunga na Yanga baada ya kumalizika kwa mkataba wake ndani ya Msimbazi.