SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 14 Novemba 2016

T media news

Kulikoni Ikulu, Serikali na CCM Wanachelewa Kutoa Majibu ya Tuhuma za Msingi Kama Hizi?

Ndugu wapendwa, kumezuka tuhuma nyingi wiki iliyopita...kwanza ilikuwa ya mhe. Mbowe bungeni, ya wabubge hupewa ten M, akanyamazishwa.

Tukasubiri tamko la chama tawala kimya, serikalini kimya, ikulu kwa rais kimya hadi leo.

Pili ishu ya kagera hakuna ufafanuzi wa maana hadi sasa tunaumizana na maswali wenyewe but serikali ipo kwa nini isije na majibu na kuondoa huu kma ni upotoshwaji wa habari kama watu wanavyodai.

Serikali hii haijawah kuwa na kigugumizi kwa swala lolote, kuna tatizo gani la mawasiliano kujibu hizi hoja, kwenye Chama Ole sendeka kimya, serikalini (waziri mkuu) kimya, ikulu (rais) wetu kimya nani wa kutupa majibu sahihi?