SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 17 Novemba 2016

T media news

KESI YA SCORPION KUANZA KUSIKILIZWA TAREHE 30

Scorpion (aliyefungwa pingu) akielekea kwenye chumba cha mahakama.



Scorpion akiwa ndani ya gari la polisi.

Ile kesi inayomkabili Salumu Njwete ‘Scorpion’ ya kupora na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili, Said Mrisho, inatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi Novemba 30, mwaka huu.


Akizungumza leo wakati akimsomea mashtaka Scorpion alipopandishwa kizimbani kwa mara nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mwendesha mashtaka  Chensesia Gavyole mbele ya Hakimu Flora Haule alisema upepelezi wa kesi umekamilika hivyo akamuomba hakimu ataje tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.



Hakimu Haule alisema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30, mwaka huu lakini Scorpion alitoa ombi kwa mahakama kwamba kutokana na kwamba upepelezi umekamilika asomewe maelezo ya awali hapohapo jambo ambalo hakimu alimwambia haliwezekani mpaka siku hiyo kesi itakapoanza kusikilizwa.



Septemba 6 mwaka huu maeneo ya Buguruni, Scorpion anadaiwa kuwa alimpora Said fedha, cheni ya dhahabu na kumjeruhi kwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni na begani ambapo kesi hiyo imekuwa ikitajwa mara kadhaa mahakamani hapo.