SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

T media news

Julius Malema Aanzisha Maandamano Kumg’oa Zuma Afrika Kusini

 PRETORIA: KIONGOZI Mkuu wa Chama pinzani cha Economic Freedom Fighters (EFC), Julius Malema leo Jumatano, Novemba 2, 2016 ameanzisha maandamano ya kumngo’a madarakani Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Ameeleza kuwa, maandamano hayo hayatakuwa na kikomo na yataanzia Church Square katikati ya Jiji la Pretoria nchini humo.

 Malema akiwa anawahutubia wafuasi wake mbele ya Mahakama Kuu Pretoria aliwaambia kuwa maandamano yatamaliza pindi watakapojisikia kuondoka, lakini hawatakuwa na nia hiyo ya kuondoka.

 Mbali na hivyo, Malema amewahataadharisha polisi na vyombo vingine vya usalama kutoingilia maandamano yao, amewaambia kazi yao ni kuhakikisha wanapatiwa usalama na si vinginevyo. Amesema hana haja ya kuomba kibali cha maandamano kutoka polisi au mahakamani kwani ni haki yake kisheria.

Amewaambia polisi yeye kama Julius Malema Kazi yake nikuandaa Maandamano na ana hakikisha yanafanyika na Polisi kazi yao ni kuwalinda. Maandamano yanaanza rasmi leo tarehe 2016 November 02 kuanzia saa 12 za asubuhi mpaka hapo Zuma atakapo achia nchi.

Amesema uhuru wa Afrika Kusini haukupatikana kirasihi halafu yeye Zuma aje waibie rasilimali zao, wakati watu wengi waliuwawa kupigania uhuru.

Hayo yamekuja kufuatia tuhuma za Bw. Zuma kuwa ni fisadi na amejimilikisha sehemu kubwa ya mali za Wasauzi.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la BBc zimeeleza kuwa, kuna ripoti mpya iiliyokamilika na itatolewa leo na aliyekuwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini humo, Thuli Madonsela, ambayo imeeleza ufisadi mwingine uliofanywa na rais Zuma.

Katika ripoti hiyo inadaiwa kuwa, mtoto wa kume wa Jacob Zuma, Duduzane aliingia kwenye biashara na kampuni maarufu ya Wahindi ya Guptas.

Ajay, Atul na Rajesh Gupta walihamia Afrika Kusini wakitokea India tangu 1993Walifanya makubaliano ya kibiashara kwenye usafirishaji, madini, nishati, teknolojia na habari.lWapinzania waliwapa jina la utani wao na rais Zuma kuwa ni “Zuptas” kutokana na ukaribu wao.Wamesema wanajiondoa kufanya biashara Afrika Kusini kutokana na matatizo ya kisiasa.Benki kubwa zimegoma kufanya nao biashara.