SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 1 Novemba 2016

T media news

Chicago Bulls sio watu wa mchezo mchezo. NBA wameishika.

Dwayne Wade, Rajon Rondo na Robin Lopez ni moja ya majina mapya katika jiji la Chicago kunako klabu ya Chicago Bulls inayoshiriki ligi kuu ya Kikapu yaani NBA. Ni majina ambayo kila mpenzi wa mchezo huu alikuwa akisubiri kuona namna gani yataungana na kufanya vitu adimu, naam nayo yamejibu.

Jimmy Butler hajasita kuwasifia wachezaji hao wageni na akiamini kuwa wataisaidia Chicago Bulls kufika mbali msimu huu.

Butler alifunga pointi 22, Wade alifunga pointi 12 ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza nje ya uwanja wa nyumbani tangu atoke katika klabu ya Miami Heat, na sasa Bulls wameanza vyema na rekodi yake kufikia 3-0 baada ya kuichapa Brooklyn Nets kwa pointi 118-88 alfajiri ya Jumanne.

Wakiwa na Dwayne Wade na Rajon Rondomaana yake ni kuwa Bulls wamerekebisha kwa kiasi kikubwa eneo lao la nyuma, na wanaonekana watakuwa na msimu mzuri wakati huu huku wakiwa atayari wamevifunga vilabu vya  Boston na Indiana kabla hawajaifunga Brooklyn Nets kwa tofauti ya pointi 33.

Nikola Mirotic alikuwa na pointi 16 na rebound 10, huku Taj Gibson akiongeza pointi 14 na kudaka rebound 11 kwa upande wa Bulls.

Bogdanovic alifunga pointi 15 huku Jeremy Lin akamaliza na pointi 14 kwa upande wa Brooklyn Nets ambao sasa wana rekodi ya 1-3.

HIGHLIGHTS