Dar es Salaam. Shule ya Sekondari ya Tegeta inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM, inadaiwa kuuzwa kinyemela kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita, ipo Tegeta, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Inadaiwa wanafunzi watahamishiwa kwingine.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema shule hiyo haijauzwa kama watu wanavyodai, bali imefidiwa na Chuo cha Mzumbe.
Chanzo cha Habari: Gazeti la Mwananchi