Leo September 26, 2016 Marekani inaingia kwenye headlines tena baada ya Mdahalo wa kwanza kati ya wagombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic na Donald Trump kutoka chama cha Republican kufanyika leo Jumatatu saa 3 usiku kwa saa za Marekani.
Mdahalo huu wa kwanza kati ya Bi. Clinton na Trump utaoneshwa kote duniani kupitia Televisheni na radio na unatarajiwa kuchukua muda wa dakika 90.
Wamarekani na watu wengine duniani watapata fursa ya kipekee kusikia kutoka kwa wagombea hao kuhusu maswala mbalimbali kama uchumi, usalama na sera zao kuhusu mambo ya nje. Wataalamu wa mambo wanatazamia kuwa Hillary Clinton mwenye umri wa miaka 68 kama mtu anayefahamu maswala mengi kuhusu uongozi baada ya kufanya kazi katika sekta ya utumishi wa umma kwa miaka 40, ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri wa Mambo ya nje.
Donald Trump mwenye umri wa miaka 70, anayaefahamika kwa utajiri wake anafahamika kama mzungumzaji mzuri ambaye wachambuzi wanaona mara nyingi amekuwa hawezi kuelekezea kwa kina maswala muhimu yanayoikumba Marekani na dunia.
Uchaguzi nchini Marekani umepangwa kufanyika tarehe 8 mwezi November, na kuelekea katika uchaguzi huo, na kwa mujibu wa kura za maoni zilizofanywa na Gazeti la Washington Post zinaonesha kuwa Clinton na Trump wanatoshana nguvu.