SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 27 Septemba 2016

T media news

MREMA AFURAHI PROF LIPUMBA KURUDI CUF,AMPONGEZA JAJI MUTUNGI KWA KUTENDA HAKI..!!!

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, amempongeza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kwa jitihada za kusuluhisha mgogoro wa uongozi uliokuwepo ndani ya Chama cha Wananchi (Cuf)Amewasihi viongozi wengine wa vyama vyote vya siasa nchini kuzingatia Katiba za vyama vyao, misingi ya demokrasia na sheria za nchi, ili kuepusha na kuondoa migogoro ndani ya vyama au kati ya chama kimoja na kingine.

Amesema hakuna kiongozi wa kisiasa aliyekamilika kwa asilimia 100 kwakuwa , kila mmoja ana udhaifu wake. Mrema alitoa pongezi hizo jana Dar es salaam kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari. Sehemu ya taarifa hiyo ilisema, " TLP inampongeza Msajili na ofisi yake kwa kutatua mgogoro huo kwa kuzingatia sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa na pia, imezingatia misingi ya demokrasia ambayo ni nguzo ya mfumo wa vyama vingi vya siasa".

Alisema chama hicho kinaamini kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haikupendelea upande wowote kama baadhi ya watu wanavyodai, bali imefanya kazi yake kwa kuzingatia sheria ya vyama vya siasa ambayo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa Msajili na sheria hiyo kukifuta chama chochote cha siasa nchini, endapo kitakwenda kinyume cha sheria hiyo, pamoja na kusuluhisha migogoro

Alisema kwa vile ofisi ya Msajili imeshatoa maelekezo kwa chama cha Cuf, ni vyema wanachama wote wa chama hicho wakatulia na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na ofisi hiyo, ili kupata suluhisho la kudumu kwa manufaa ya chama chao na kwa manufaa ya taifa.