Kuna nyumba ilikuwa sokoni inayofanana na ile Diamond amedai kuinunua South, zinafanana tu ama ni ile ile? Hilo ni swali ambalo hadi sasa wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini sasa Bongo5 ina jibu la uhakika.
Wiki iliyopita Diamond Platnumz alitengeneza vichwa vya habari baada ya kupost kwenye Instagram picha ya nyumba anayodai ameinunua nchini Afrika Kusini itakayotumiwa na mchumba wake Zari.
Picha hiyo aliisindikiza na maelezo mazito yaliyowalenga wale aliowaelezea kama wanaopenda kujisifia ni matajiri na kumuita yeye maskini ilhali watoto wao bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga. Wengi walitafsiri kuwa dongo hilo lilimlenga ex wa Zari, Ivan anayefahamika kwa kuishi maisha ya kifahari.Hata hivyo, muda mfupi baada ya Diamond kuweka picha hiyo, wametokea watu ambao wamesambaza picha ya nyumba nyingine inayofanana kwa karibu asilimia 100 na nyumba ile iliyowekwa kwenye mtandao wa privateproperty.co.za na hivyo kuzusha minong’ono mingi.
Kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam, nyumba hiyo imelipiwa Alhamis iliyopita na tayari ni mali ya muimbaji huyo wa Salome na amefafanua kwanini bado haijatolewa kwenye tovuti hiyo.
“Nyumba imelipiwa thursday haiwezi toka muda huo huo kwenye website mpaka agency amalizane na mwenye nyumba then process zote zikamilike ndio inatolewa kwenye site,” Sallam ameiambia Bongo5.
Nyumba hiyo ipo Moreleta Park, mjini Pretoria.
Ina vyumba vitano, lounge 3, mabafu matatu, bwawa la kuogelea, balcony, gereji mbili na nyumba ya pembeni ya kuishi wafanyakazi.
Ipo kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba, 1068.
Bei yake si haba, ilikuwa inauzwa kwa Rand 2,480,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 396 za Kitanzania.
Kuhusu anachokisema Diamond baada ya watu kudhani kawapiga changa la macho watanzania, Sallam amejibu, “Anachukulia kawaida, ni mengi kila siku yanasemwa.”
Hiyo ni sababu kubwa staa huyo ameamua kujizawadia mapumziko mahsusi visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.
UPDATES:
Kibao cha ‘SOLD’ kimeshaweka kwenye nyumba aliyonunua Diamond, Pretoria, Afrika Kusini na tayari imeshatolewa kwenye listings za mtandao wa http://www.privateproperty.co.za. Na sasa ni mali yao halali..
Source:Bongo5