Kuna video imeenea kwenye mitandao ya kijamii baada ya mechi ya kirafiki wakati wa pre-season kati ya Chelsea dhidi ya Real Madrid iliyopigwa huko Michigan, Marekani.
Chelsea ilipoteza mechi hiyo kwa kufungwa bao 3-2 iliyochezwa mbele ya umati wa watu zaidi ya 105,000 idadi kubwa kuwahi kuishudia The Blues wakiwa uwanjani.
Licha ya goli safi la dakika za lala salama lililofungwa na Eden Hazard abaye alifunga magoli yote mawili, lakini baada ya mchezo Diego Costa akazua mjadala kwa mashabiki.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Brazil hajacheza mechi yeyote katika mechi mbili zilizopita za pre-season na anafanya tetesi za kutaka kurejea Hispania kuzidi kushika kasi.
Kama ilivyokawaida pale timu kubwa zinapocheza, kila sehemu ya uwanja wa Michigan hufungwa camera.
Camera zilimnasa Diego Costa wakati akiwa uwanjani akiulizwa kama angependa kurudi Madrid kwenye klabu yake ya zamani Atletico. Ambapo mshambuliaji huyo wa Chelsea alijibu kwa ishara ya kidole.
Baada ya kipigo cha 3-2 kutoka kwa Real Madrid, boss wa Chelsea Antonio Conte alithibisha kwamba, Costa atarejea Stanford Bridge wakati wowote.
Kinachoshangaza kwa sasa ni namna ambavyo jamaa hawa wawili Sergio Ramos na Diego Costa walivyokuwa karibu.
Wawili hao walikuwa kwenye battle kubwa wakati wa Mdrid derby wakati Ramos akiwa Real kipindi Costa akiwa Atletico.
Inaonekana wazi Ramos anamuuliza Costa “kwanini usirudi?” huku Costa akionekana kujibu “hawatakubali kuniachia.”
Halafu Ramos anaitaja Atletico Madrid kuhusu kumsajili Kevin Gameiro kutoka Sevilla kabla ya kuendelea na mazunguzo mengine.
Wakati akizungumza na mashabiki wa Chelsea, Costa pia alithibitisha kwamba Chelsea haiwezi kumruhusu aondoke.
Full video ya stori za Sergio Ramos na Diego Costa