SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 2 Agosti 2016

T media news

TFF NI WAKALA WA VILABU?

Na Isack Makundi, Babati -Manyara

TFF kirefu chake ni Tanzania Football Federation, kwa muda mrefu nimekuwa  nikisikia mvutano juu ya mapato kati TFF na vilabu hasa hivi vikubwa (Yanga na Simba) kuwa vinapunjwa kwenye mgao.

Mechi namba 117 ya 2014/2015 iliyowakutanisha Simba na Yanga zilipatikana shilingi milioni 436,756,000 TFF Sh.20,015,016.20 na Bodi ya Ligi (TPLB) Sh. 26,686,688.27,  klabu ya Simba Sh. 115,086,343 (34.5%) huku Yanga wakipata Sh.81,727.83 (24.5%)

Na nukuu: Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya Sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% Sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji Sh. 17,415,300, FDF TFF Sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600. Mgao wa Uwanja Sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo Sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) Sh. 26,686,688.27, TFF Sh. 20,015,016.20, DRFA Sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba Sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata Sh. 81,727.83. mwisho wa kunukuu.

Kuna mkataba wa miaka 3 kati ya Vodacom na timu za ligi kuu Tanzania, billion 6.6 yaani billion 2.2 kwa mwaka, kuna mkataba wa miaka 5 kati ya Azam TV na timu za ligi kuu Tanzania billion 23 yaani billion 4.6 kwa mwaka.

Mkataba wa Vodacom hauzidi million 50 x 16 = milioni 800 jumlisha na zawadi assume million 500 jumla kuu billion 1.3 baki million 900.Azam TV 4.6 billion kwa mwaka, kila timu million 126 pamoja na zawadi kwa kila timu million 40 jumla 166 x 16 = billion 2.656 kwa mwaka (4.600-2.656= 1.944B)Fedha baki TFF, Vodacom million 900 + Azam TV 1.944 + million 400 za FIFA = billion 244

Kwa maana hiyo kila timu inapata fedha za Azam million 166 + Vodacom 81.25= 247.25 hapo nimetafuta wastani ikiwa pamoja na zawadi zote, ukizidisha kwa timu 16 unapata billion 3.956 kati ya billion 6.8 (6.8 -3.956 =2.8 billion) + million 400 FIFA = 3.2 Billioni.

Swali langu kati ya TFF na vilabu nani anayebeba mzigo mkubwa? Hapo nimeacha mapato ya milangoni n.k.

Vilabu vinalipa mishahara wachezaji, makocha, usajili, posho kambi na wafanyakazi/watumishi ambapo ni mzigo mzito sana. Mara nyingi nasikia TFF wanajitetea kuwa wana mzigo wa timu ya taifa na timu ya vijana. Vilabu navyo vina timu kubwa na timu za vijana, hapohapo TFF hawalipi mishahara wala kusajili wao ni posho tu.

Kocha wa timu ya Taifa alikuwa analipwa na wizara ya Habari na Michezo (J.M Kikwete) japo sijui kwa sasa. Makocha wa timu za taifa hawazidi 10, kambi zinafanyika mara 1 kwa miezi 2 au zaidi, wakati vilabu kwa mwaka miezi 11 yote inakuwa na wachezaji zaidi ya 22 wanalipwa mishahara, posho, bima, mifuko ya jamii, fedha za usajili, n.k. Hapa kuna tatizo vilabu vinatakiwa kuwa na umoja ili wapate angalau 80% ya mapato yote ambapo ni billion 5.52/16 yaani kila klabu million 345 kwa mwaka. Kwenye mapato ya milangoni anayefaidi ni TFF (TFF Sh. 20,015,016.20 na Bodi ya Ligi (TPLB) Sh. 26,686,688.27). TFF na bodi ya ligi ni kitu kilele (baba na mtoto) mechi moja wanaondoka na zaidi ya million 46 kwa siku. Timu moja hucheza mechi 30 kwa mwaka, kwa timu 16 ni mechi 480 hata kama kila mechi wanachukua 30 (TFF na Bodi ya ligi) kwa mwaka ni billion 1.44 a lot of money. Sikushangaa TFF walipoamua kwenda kupanga PFF tower mwaka 2014 mpaka FIFA ikaingilia kati maana fedha zipo za kutosha. Ni kutafuta tu justification ya matumizi huku timu zinaumia.

Wadhamini wote hawa Azam TV, Vodacom n.k wanakuja sababu kuna vilabu, lakini vilabu visusie ligi na TFF iwepo tuone kama wataendelea kuwepo. TFF inaweza isiwepo vilabu vikawepo na wadhamini wakaendelea kuwepo, lengo lao kujitangaza kibiashara.

Sikatai kuna mazuri ambayo TFF wanafanya lakini hili la mgao wa fedha kwa vilabu nawapinga kwa nguvu zote siyo fair hata kidogo.

Jerry Murro kuna mambo ambayo nilikuwa namkubali kama kupigania maslahi ya timu na kama kungekuwa na support kutoka timu zingine nadhani TFF wangeelewa somo.

Mpaka najiuliza TFF ni wakala wa vilabu? Maana anayefaidi ni yeye kuliko vilabu. Vilabu unganeni mpiganie haki yenu tunataka mpate fedha ligi yetu iwe na ushindani wa kweli.