SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 2 Agosti 2016

T media news

NUH MZIWANDA AKODI BODIGADI KISA KIPIGO,MAZITO YAFICHUKA


 

Stori: Gabriel Ng’osha
KUFUATIA kuwepo madai kuwa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda kutishiwa kupewa kichapo na mijemba inayodaiwa ilitumwa na aliyekuwa mpenzi wake Shilole, hatimaye Nuh aamua kukodi bodigadi wa kumlinda.
Nuh alionekana akiwa na bodigadi huyo kwenye Tamasha la Mwendokasi lililofanyika Viwanja vya Posta jijini Dar hivi karibuni jambo lililozua minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake.
Katika tamasha hilo burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba, Isha Mashauzi, Juma Nature, Rich One, Man Fongo, G. Nako, Lord Eyes, Navy Kenzo, Snura, Nay wa Mitego ziliwapagawisha mashabiki.