SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Agosti 2016

T media news

PICHA ZA UFUNGUZI WA DR NTUYABALIWE FOUNDATION YA JACQULINE MENGI(+VIDEO)

Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akifungua maktaba hiyo

Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi, Alhamisi hii amezindua taasisi yake, Dr Ntuyabaliwe Foundation kwa kuikabidhi shule ya msingi Kinondoni maktaba ya kisasa ambayo imefanyiwa ukarabati na taasisi hiyo.

Akiongea katika uzinduzi huo, Jacqueline amesema kuwa ameamua kukarabati maktaba hiyo ili kuwapa wanafunzi motisha wakupenda kujisomea vitabu.

“Tunashukuru Mungu leo tumekabidhi maktaba ambayo imekarabatiwa na Dr Ntuyabaliwe Foundation, lakini vilevile tumekabidhi vitabu ili kuanzisha na kuendeleza hii maktaba. Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe Foundation iliundwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Baba yangu Dr Ntuyabaliwe ambaye kwa sasa hayupo tena. Watu walimfahamu Dr Ntuyabaliwe kama daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, lakini watu walimfahamu kwa ukaribu zaidi kama Baba alithamini sana elimu na alipenda sana kuhimiza watu kusoma vitabu,” alisema Jacqueline.

Aliongeza, “Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe ina lenga kuhamasisha watu kusoma vitabu kwa watoto wadogo. Lengo letu kubwa ni kudumisha utamaduni wa kupenda kujisomea siyo kujisomea kwa ajili ya kufanya mtihani, lakini kujisomea kama utamaduni ambao utakusaidia katika kujiendeleza, kwa hiyo taasisi hii itafanya kila jitihada kuhakikisha watoto wanapata vitabu vya kutosha,”

Kwa upande wa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda, ameipongeza taasisi ya Dr Ntuyabaliwe Foundation kwa kuisaidia serikali katika kuboresha elimu.


Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi akimuonyesha baadhi ya vitabu Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda

Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi akisoma vitabu

Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi akizungumza na wanafunzi

Jacqueline Mengi akiwa na rafiki zake