SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 26 Agosti 2016

T media news

Mfanyabiashara Ataka Kujirusha Daraja la Ubungo

Katibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha, akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa haki.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha.

Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni Mtanzania anahitaji haki ndipo walimsubiria alipokuwa akimpa mkono ndugu yake kama ishara ya kumuaga wakamvuta na kufanikiwa kumshusha.

Baada ya kushushwa, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo wafanyabiashara wenzake  walidai kwamba alikuwa na mgogoro na mwenzake waliyekuwa wanafanya biashara pamoja. Hata hivyo, hadi mwandishi wetu anaondoka kituoni hapo, jamaa huyo alikuwa akitoa maelezo.

Stori/picha: Gladness Mallya/GPL