SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 26 Agosti 2016

T media news

Majibu sahihi kwa Charles Kitwanga juu ya Ndege Mpya za ATCL

Na Rashid Chilumba

Charles Kitwanga mwanasiasa aliyefutwa kazi ya uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi kwa sababu ya ulevi uliopindukia ameibua mjadala wa kichekesho leo katika mitandao ya kijamii.

Gazeti moja la kila siku limemkariri Kitwanga akikosoa uamuzi wa serikali ya John Magufuli wa kununua Ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q400 kwa lengo la kufufua Shirika la Ndege la Taifa.

Kitwanga amecharuka wakati wa vikao vya kamati za bunge na kutoa taarifa za uongo na upotoshaji kuhusu ununuzi Huo wa Ndege hizo za serikali.

Amepata mashabiki wengi tu leo wale wasiotutakia mema.

Nitayadurusu madai moja moja ya kitwanga na kuyatolea majibu ili kumzuia kitwanga asihamishie MSONGO wake wa mawazo katika masuala yenye manufaa kwa taifa.

#HOJA

Kitwanga anadai Q400 ni Ndege zisizo na Mwendo

#JIBU

Sijui Kitwanga amesoma shule gani ambayo hailumfundisha hata kufanya utafiti, na sielewi anazilinganisha Q400 na Ndege zipi hadi adai hazina mwendo?

Kwanza lazima Kitwanga aelewe kuwa serikali imepanga kununua Ndege tatu kwa mwaka huu wa fedha, mbili ni Q400 (anazoponda Kitwanga) na moja ni C300.

Ndege mbili ndogo za Q400 zinanunuliwa mahsusi kwa ajili ya safari za ndani ni eneo jirani kama visiwa vya Comoro na Moja kwa ajili ya masafa marefu.

Hivyo ili kujua kama Q400 ni Ndege sahihi kwa matumizi yaliyopangwa ni lazima kuzifahamu Ndege zenyewe na kuzifananisha na Ndege nyingine za aina na mtindo wa Q400.

SASA Q400 NI NDEGE YA AINA GANI?

Q400 ni Ndege ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 70 hadi 84. Q400 ina uwezo wa Kwenda umbali wa nautical miles 1000 Sawa na 1852 Km bila kutua kwa safari moja ikiwa na Tani Saba za Mizigo (Kilogram 7000).

Pia ina uwezo wa Mwendokasi wa hadi 360 knots (maili 414 kwa saa).

Sasa kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, Spidi hiyo ya Q400 ni kubwa kwa zaidi ya knots 110 dhidi ya Ndege nyingine za aina yake zinazotumia pangaboi ikiwemo ATR zinazotumiwa na kampuni kama Precision Air ambazo Spidi yake ni Kati 200-250 knots kwa saa.

Sifa za hapo juu za Q400 zinaifanya kuwa na uwezo unaokaribiana wa Upinzani na Ndege aina ya Jets kama Airbus 319 inayotumiwa na Fastjet ambazo Spidi yake ni 400-450 knots pekee. Hivi simulizi za kitwanga kwamba Ndege zilizoagizwa na serikali hazina kasi ni Upuuzi unaotokana na MSONGO wake wa mawazo.

Q400 haishindani na Ndege za wajihi wake bali Ndege kubwa kama Airbus 319.

Pia jambo la nyongeza ni kwamba Q400 inatoa unafuu mkubwa katika matumizi ya mafuta na matengenexo ikilinganishwa na jets kama Airbus za Fastjet kwa safari inayofanana.

Hivyo kutumia Q400 kwa safari za ndani ni bora kwa Ufanisi na gharama ndogo mno kuliko aina nyingine yoyote ya Ndege katika soko la dunia.

Na kwa sisi tunafufua shirika letu la Ndege taratibu kwa kuanza na huduma za ndani zilizoboreka, kisha unajenga imani ya shirika katika usalama na uhakika kwa abiria na unafuu wa uendeshaji kabla hujakimbilia kununua Ndege kubwa ambazo ni ghali kuziendesha na kuzihudumia Q400 ni chaguo sahihi kabisa kwa kila sifa.

Hivyo Kitwanga masuala ya Ndege muachie Rais Magufuli.

#HOJA2

Kitwanga anadai Kampuni ya Bombardier ni ndogo na ya mtu binafsi hivyo ni kosa kununua Ndege huko.

#JIBU2

Hiki ni kichekesho kipya cha Dogo na Oscar Makoye.

Hivi Kitwanga anaposema Bombardier ni kampuni ndogo ya mtu binafsi anatoa wapi taarifa zake? Ulevi ni nomaa.

Kwanza Kitwanga lazima afahamu kampuni zote kubwa duniani za Ndege kwa maana ya Boeing, Airbus na Bombardier zilianzishwa Na zinamilikiwa na mabunyenye wenye fedha hivyo ni kituko kwa mtu wa hadhi ya kitwanga kudai kuwa hatupaswi kununua Ndege Bombardier kwa sababu inamilikiwa na mtu binafsi. Sasa alitaka kampuni imilikiwe na kifaru
? Hivyo Hoja Hii ni ya kipuuzi.

Na Hoja kuwa Bombardier ni kampuni ndogo ni ya aibu, Bombardier ilianzishwa mwaka 1942 huko Canada Miaka Karibu 20 kabla Airbus moja ya kampuni kubwa duniani za Ndege haijaanzishwa mwaka 1970 (Yaan wakati Bombardier inaanzishwa mwanzilishi wa Airbus pengine alikuwa Ndiyo anachora chora picha za Ndege kwenye makaratasi.

Ukubwa wa kampuni ya Bombardier Sio tu unatibitishwa kwa ukongwe wake bali pia unaweza kuthibitishwa na wingi wa wafanyakazi ambao unalingana na kampuni nyingine kama Airbus.

Bombadieir kitengo cha Ndege pekee kina wafanyakazi 65,698 kwa takwimu za mwaka 2011 wakati Airbus na vitengo vyake vyote ikiwemo na kile cha treni ina jumla ya wafanyakazi 73978.

Linganisha mwenyewe hapo kabla sijaweka kitengo cha treni cha Bombadieir wafanyakazi wake. Sasa ni udogo upi anaouzungumzia Kitwanga? Au chupa yake ya bia? Kitwanga umelewa.

#HOJA3

Kitwanga anadai ATCL Ndiyo itakuwa kampuni ya kwanza ya Ndege kutumia Ndege aina ya Q400

#JIBU3

Ukitaka kujua Kitwanga ni mlevi na alistahili kufukuzwa kabla hajaiba gobole la polisi na kuanza kutembea nalo mtaani ni katika hili.

Kwanza inaonekana haelewi chochote kuhusu Ndege huyu jamaa, tangu Q400 izindulewe mwaka 1983 Ndege za aina hiyo zaidi ya 1000 zimeundwa. Takwimu za karibuni zinaonesha kuwa kampuni 43 za Ndege duniani ikiwemo American Airways, shirika la Ndege la taifa la Marekani linatumia q400.

Air Tanzania itakuwa ni mteja wa 44 tena mwenye order ndogo ya Ndege mbili tu. Jazz Air kampuni ya usafiri wa anga ya nchini Canada imetoa odred ya Q400 10 mwaka Jana.

Lakini wakati huo huo kampuni nyingine 29 za Ndege duniani zimetoa oda ya kutengenezewa
Q400 zinazofikia 102 ikiwemo kampuni kubwa ya Ethiopian Airlines na Westjet ya Marekani. Ulevi nomaa.

Sasa Kitwanga aliposema sisi Ndiyo tutakuwa wa kwanza kutumia Q400 alikuwa mzima au tayari alikuwa amepiga masangati?

Hitimisho

Kitwanga na wapuuzi Wengine msioelewa mambo pumzikine na mumuache Rais Magufuli afanye kazi tuliyomtuma.

Ushauri kwa Ndgu Kitwanga ni kupeleka maji na huduma za afya jimboni.

Endelea kuisoma namba

#KaaChonjo #TufanyeKazi #AndamanaUkione

By Weston Songoro